|

IMFSL DISCLAIMER

RUSHWA NA BIASHARA HARAMU

Imarisha Maisha Financial Services Ltd inapenda kuutarifu umma kwamba itaendelea kutekeleza majukumu yake kwa kufuata taratibu zote na sheria za nchi na pia haijawahi na haita jihusisha na vitendo vya ujangili, rushwa, madawa ya kulevya wala biashara yoyote ile ya magendo (Haramu) au kusapoti(kusaidia) vitendo hivyo. Hivyo basi Imarisha Maisha Financial Services Ltd inatoa onyo kali kwa mteja au mfanyakazi wake yeyote atakae bainika kujihusisha au kuihusisha kampuni ya Imarisha Maisha Financial Services Ltd na vitendo hivyo. Kampuni inaahidi kutoa ushirikiano wa kutosha endapo itagundua njama zozote zinazoashiria uvunjifu wa sheria kwenye vyombo vya usalama ili wahusika wachukuliwe hatua za kisheria.

MITANDAO YA KIJAMII

Kurasa katika mitandao ya kijamii ya Imarisha Maisha Financial Services Ltd yaani Facebook na Instagram imeundwa na kusimamiwa na Imarisha Maisha Financial Services Ltd. Hivyo basi, Link zilizopo katika maudhui au tovuti zingine mtandaoni hazipaswi kuchukuliwa kama ushirika baina ya tovuti hizo na Imarisha Maisha Financial Services Ltd. Imarisha Maisha Financial Services Ltd haiwajibiki na haitawajibika na maudhui yaliyomo kwenye tovuti hizo. Maoni au mitazamo inayotolewa kupitia mitandao ya kijamii ya Imarisha Maisha Financial Services Ltd na majukwaaa mengine ya mtandaoni ni ya wafanyakazi, watu binafsi, wateja na washiriki wengine na si lazima yaambatane au kulenga sera au utendaji wa Imarisha Maisha Financial Services Ltd. Imarisha Maisha Financial Services Ltd inahimiza ushiriki wa watu mtandaoni na utoaji wa maoni ya heshima kwenye tovuti yake na kurasa zake za kijamii.

Imarisha Maisha Financial Services Ltd ina haki ya kuondoa maudhui yoyote yaliyochapishwa kwa sababu yoyote kama vile: Maudhui ya kutisha, yenye picha chafu, ukiukaji wa haki miliki au haki za faragha, zilizo nje ya mada, zinazolenga biashara au ukuzaji wa ushirika au programu zisizohusiana(kufanania) na zile za Imarisha Maisha Financial Services Ltd, au Haramu, Maudhui inayojumuisha lugha chafu au matusi.

Hili halitavumiliwa. Kuheshimiana kunahimizwa sana wakati wote, hata wakati wa kutokua na maelewano. Kila mtu anatakiwa kuwajibika kikamilifu kwa maudhui anayochapisha kwenye ukurasa wowote wa mtandao wa kijamii wa Imarisha Maisha Financial Services Ltd.

Sheria za kuzingatia:

  • Link au maoni yaliyo na maudhui ya ngono hayaruhusiwi
  • Maudhui yanayolenga kutoa siri za kampuni hayaruhusiwi
  • Haupaswi kutumia kurasa za mitandao ya kijamii za Imarisha Maisha Financial Services Ltd kutangaza biashara zako au kurasa zako
  • Maudhui yanayolenga kutangaza au kusapoti(kuunga mkono) biashara haramu au rushwa hayaruhusiwi
  • Maudhui yanayolenga maswala ya kisiasa hayaruhusiwi
  • Tuma(chapisha) maoni yenye maana na yenye heshima - matamshi ya kuudhi, ya kibaguzi au ya kukashifu hayaruhusiwi
  • Nyenzo zote zinazochapishwa au kutumika lazima ziheshimu hakimiliki ya wahusika wengine
  • Maudhui yoyote ambayo yanachukuliwa kuwa yasiyofaa yataondolewa bila taarifa
  • Imarisha Maisha Financial Services Ltd ina haki ya kumzuia (kum-block) mtumiaji kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii kwa ukiukaji wowote wa Sheria na Masharti yaliyo hapo juu

Kwa kuwasilisha maudhui kwenye tovuti au kurasa yoyote ya mitandao ya kijamii ya Imarisha Maisha Financial Services Ltd, mtumiaji anaelewa na kukiri kwamba taarifa hii itapatikana katika umma, na kwamba Imarisha Maisha Financial Services Ltd inaweza kutumia taarifa hiyo kwa madhumuni ya utangazaji au uboreshaji wa huduma zake ndani na nje. Tafadhali kumbuka kuwa watu au tovuti zingine zinaweza kutumia taarifa zilizochapishwa nje ya uwezo wetu. Watumiaji ambao hawataki taarifa walizotoa kupitia tovuti au kurasa zetu kutumika, kuchapishwa, kunakiliwa na/au kuchapishwa tena, hawapaswi kushiriki katika mijadala ya mtandaoni katika kurasa za kijamii za Imarisha Maisha Financial Services Ltd

Imarisha Maisha Logo