Huduma za Mikopo

Imarisha Maisha inajihusisha na mikopo ya aina tatu (3). Aina hizo ni Binafsi, Wafanyakazi na Vikundi. Pata ufafanuzi zaidi wa kila aina ya mikopo tulionayo

Mikopo Binafsi

Imarisha Maisha inatoa mikopo hii kwa mtu binafsi ndani ya nusu saa baada ya nyaraka zote muhimu kukubaliwa. Mkopaji anatakiwa kuwa na dhamana zenye thamani kulingana na mkopo anaochukua na kuendelea. Mkopo huu utarudishwa ndani ya mwezi mmoja (1) tu au zaidi kutokana na makubaliano na uanzia kiasi cha laki tano 500,000/= hadi milioni thelathini 30,000,000/=. Pamoja na riba yake kwa asilimia husika.

Mahitaji Yake ni kama yafuatayo;

 1. Nakala ya kitambulisho cha mpiga kula .
 2. Barua ya utambulisho wa mwenyekiti wa mtaa .
 3. Barua ya afisa mtendaji wa kata.
 4. Mdhamini mmoja mke/mme .
 5. Nyaraka halisi za dhamana.
 6. Nakala1 ya official search .
 7. Picha nne (4) za mdhamini.
 8. Picha nne (4) za mhusika

Mikopo ya wafanyakazi

Mkopo huu unatolewa kwa haraka, ndani ya dakika 15 pale unapokuwa umekamilisha nyaraka zote ofisini na kufanyiwa uwakiki wa nyaraka zako na ofisi kujilizisha. mkopo huu huanzia elfu hamsini (50,000/=) hadi milioni tano (5,000,000/=) kutokana na utakavyokuwa umemaliza mkopo wako na urejeshaji sahihi Mkopaji atatakiwa kurudisha pesa aliyokopa pamoja na riba ya asilimia husika ndani ya mwezi mmoja tu. Kufanya udanganyifu dhidi ya ofisi utachukuliwa hatua kali za kisheria pamoja na kufikishwa mahakamani na kulipa gharama zote za usumbufu.

Mahitaji Yake ni kama yafuatayo

 1. Nakala moja ya kitambulisho cha mpiga kura.
 2. Nakala moja ya kitambulisho cha kazi .
 3. Barua ya utambulisho kutoka ofisini
 4. Benki statimenti ya benki husika mshahara unakopita miezi (3) ya tarehe za karibu
 5. utambulisho kwa mwenyekiti wa mtaa
 6. Picha mbili (2)

Mikopo ya Wafanyabiashara

Imarisha Maisha inatoa mikopo hii kwa mfanyabiashara/wafanyabiashara. Mkopo huu utulewa kwa haraka na utalipwa ndani ya miezi mitatu (3). Mkopoji anezapata mkopo kuanzia laiki 5 (500,000/=) hadi milioni thelathini (30,000,000/=). Mkopoaji anatakiwa ajihusishe na biashara ambayo iko rasmi na iliyosajiliwa kama chanzo cha mapato yake.

Mahitaji Yake ni kama yafuatayo

 1. Leseni ya biashara.
 2. TIN ya malipo.
 3. Aache dhamana kama gari,pikipiki au bajaji pia hati ya kiwanja
 4. Nakala moja ya utambulisho wa mwenyekiti wa mtaa .
 5. Nakala ya kitambulisho cha kura au taifa.
 6. Picha mbili (2) .
 7. Mdhamini mmoja (mke / mme).